Posted by Williammalecela.com on Tuesday, November 08, 2016
 |
Miaka mitano iliyopita mwanamke
mwenye umri wa zaiid ya miaka 50 aliyekuwa akiishi kwenye jengo moja la
miaka 87 mjini Mumbai alipata umaarufu mjini humo kwa kupinga mradi wa
tajiri Donald Trump.
Taarifa zilimuelezea Smita Panvalkar ambaye
alikuwa akiishi na mmewe , mtoto wake wa kiume na nduguye katika ghorofa
ya kwanza ya jengo hilo, kama kizuizi kikubwa cha Trump alipokuwa na
mpango wa kuanza mradi wake wa kwanza nchini India. |
Mwaka 2011 Trump, mfanyibiashara tajiri aliungana na mfanyibiashara
mwingine raia wa India kujenga jumba la ghorofa 65 la Trump Tower lenye
vyumba 50 vya kifahari.
Mji wa Mumbai unakumbwa na ubaha mkubwa wa
ardhi, na mijengo yoyote mipya hujengwa baada ya majengo ya zamani
kubomolewa kwa kuwalipa fidia au kuwapa makao mapya wakaazi wa zamani.
Hatma ya jengo la ghrofa la Pathare Prabhu ambapo Panvalkars alikuwa akiishi tangu mwaka 1990 ilikuwa hatarini.
 |
" Tuliishi masha ya kawaida hadi mwaka 2011, alisema Prasad Panvalkar ambapo alikuwa akilipa kodi ya dola 2.7.
Haikuchukua
muda mrefu kabla ya Trump na mfanyibiasahara wa India kuafikia
makubaliano ya kujenga jumba la Kwanza la Trump Tower nchini India.
Hata hivyo Smita Panvalkar alikataa kuondoka kabisa. |
 |
Matajiri hao walitoa fidia. Lakini Smita akasema kuwa hataondoka kamwe hadi apewe chumba ndani ya jengo jipya.
Kwa
miaka sita iliyofuata hadi mwezi Juni mwaka huu, familia ya Panvalkars
ilikataa kuondoka na kutatiza jitihada za kubomolewa kwa jengo hilo. |
Mradi huo mpya ulikumbwa na changamoto zaidi na hata kushindwa kufuata sheria za ujenzi.
Mwaka 2013 aliachana na mradi huo.
0 comments:
Post a Comment