KWA kawaida binadamu yeyote huzaliwa na kubatizwa jina ambalo hulitumia katika masomo na hata kazi yake.
analizoea jina hilo jipya na kulifanya kuwa kama rasmi. Leo Amani linakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao majina waliyopewa na wazazi wao ‘yamekufa’, hawayatumii kabisa: LULU
Jina
lake halisi ni Elizabeth Michael, Lulu lilizoeleka kupitia tasnia ya
uigizaji. Alianza kulitumia wakati alipojiunga na Kundi la Sanaa la
Kaole.
Hadi leo hii, siyo rahisi kabisa mtu kutokea na kumuita jina la Elizabeth, wengi wanamfahamu kwa jina la Lulu.
RAY
Ray
ndiyo jina ambalo limezoeleka na wengi. Vincent Kigosi alilopewa na
wazazi wake ni kama limekufa. Kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu
alipokuwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole hadi sasa.
Jina
la Ray ndiyo watu wanalolifahamu zaidi ingawa hivi karibuni baadhi ya
wasanii wenzake wamekuwa wakijaribu kumuita Vincent ili kurudisha uhai
wa jina hilo.
JOHARI
Jina
lake halisi ni Blandina Chagula. Johari lilizaliwa kwenye Tamthiliya
iliyobeba taito ya jina hilo. Akiwa katika Kundi la Kaole, alianza
kujiita Blandy, baadaye alibadilisha jina hilo na kuwa Johari
walipoingiza tamthiliya hiyo ambayo pia ilizaa filamu.
“Kuna wakati huwa najuta kutumia jina la a.k.a ambalo limefunika kabisa jina langu la asili,” anasema Johari.
DK. CHENI
Ameanza
gemu kitambo, tangu Kundi la Splended. Jina alilopewa na wazazi wake
ni Mahsein Awadhi, kwa sasa limekufa. Hakuna anayelitumia, hata yeye
mwenyewe.
Jina
hilo lilizaliwa baada ya mazoea yake ya kupenda kuvaa cheni kubwa
kwenye michezo iliyokuwa ikirushwa Runingani, kwa sasa wengi wanashindwa
hata kulitamka jina lake.
ODAMA
Jina
lake halisi ni Jenniffer Kyaka, limekufa kabisa kwa sasa. Wengi
wanamfahamu kama Odama jina ambalo alilipata kwenye filamu iliyoitwa
Odama miaka sita iliyopita
Tangu ilipotoka filamu hiyo hadi leo, jina la Odama limegeuka kuwa ndiyo la asili.
BATULI
Jina
alilopewa na wazazi wake ni Yobnesh Yusuf lakini wengi hawalijui.
Alianzia kuigiza katika Kundi la Kaole. Alianza kujiita Nesh, baadaye
akabadilisha na kujiita Batuli baada ya kucheza filamu ya ‘Fake Smile’
ya marehemu Steven Kanumba.
Toka
hapo, watu wote wakamfahamu kupitia jina la Batuli, wachache sana
wanaolijua jina la Yobnesh, zaidi ni ndugu zake wa karibu.
JB
Majina mengi ya a.k.a ameitwa. Aliitwa Bonge la Bwana, Mtumishi, Eric Ford na mwisho jina la JB likasimama katika akili za watu.
Mwenyewe anasema jina la JB analipenda sana, kuna wakati hata yeye huwa anasahau kabisa kama anaitwa Jacob.
NORA
Jina
lake halisi ni Nuru Nassoro. Takriban miaka kumi iliyopita baada ya
kujiunga na Kundi la Kaole, jina la Nuru limekufa kabisa.
Familia yake nzima wanatumia jina la Nora na si Nuru tena, amelikubali na analipenda kutoka moyoni mwake.
RICHIE RICHIE
Huyu naye ni msanii wa muda mrefu, jina lake halisi ni Single Mtambalike. Wengi hawalifahamu jina lake halisi.
Wanamuita
Richie Richie utadhani ndiyo alilopewa na wazazi wake, jina hilo
alipewa takriban miaka kumi na tano iliyopita akiwa na Kundi la Nyota
Ensembles.
CATHY
Huyu
anaitwa Sabrina Rupia, Cathy lilikuja katika michezo kipindi hicho
akiwa katika Kundi la Nyota Ensembles. Limeendelezwa hadi leo na kipo
kizazi ambacho hakilifahamu kabisa jina la Sabrina zaidi ya Cathy.
0 comments:
Post a Comment