MKONGWE
wa muziki wa bongo fleva Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ amewataka wasanii
kubadilika kwa kuimba nyimbo ambazo ni rafiki kwa utamaduni wetu ili
kulitangaza taifa.
Mb Dog alipofanya
mahojiano na gazeti la wiki la JAMHURI ameeleza kuwa muziki wa sasa upo kwa
ajili biashara na sio burudani kama ilivyokuwa kipindi cha miaka iliyopita
walichokuwa wakiheshimu utamaduni wa Kitanzania.
Anasema
kuwa sio jambo jema katika tasnia ya muziki kufanya hivyo, kwani tunaweza
kuupoteza utamaduni wetu na kuanza kuutafuta tena hapo baadaye bila mafaniko
yoyote.
“Asilimia kubwa
tumekuwa tukiiga utamaduni wa wenzetu na kuziacha za hapa nyumbani. Hali hiyo
inachangiwa na muziki kuwa ni biashara”.alisema
Mb Dog amekiri
kuwa kimya kwa muda mrefu ambapo kumechangiwa na kuhama kwake Tip Top kwenda QT,
ambako ilichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kurekodi kwa muda mrefu.
“Ni
kweli sikutoa ngoma kwa muda mrefu lakini hali hiyo imetokea baada ya kutoka
Kampuni ya Tip top Connection kwenda QT kumechangia kutorekodi kwa muda mrefu”alisema
Mb Dog.
Mb Dog
ambaye kwa sasa yupo kwenye lebel cha QS Mhanda Entertainment anaaendelea na
kazi yake ya muziki ambapo anafanya maandalizi ya kutoa nyimbo mpya aliyoifanya
kwa Man water.
“Zipo
nyimbo nyingi ambazo natarajia kuzirekodi na baada ya kukamilika nitaziweka
bayana kwa mashabiki”.

0 comments:
Post a Comment