Miss
Universe 2016 na mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimach
amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano ya mapenzi akidai kuogopa
kuharibiwa malengo yake.
Akiongea
na Bongo5 Jumamosi hii, Jihan amesema wasichana wengi wanaaribika
kutokana na ‘kiki’ pamoja na mambo yakubadili wanaume kila mara
wakiamini wanapata kiki.
“Mimi
sio mtu wa ‘kiki’ na sipendagi skendo naona kama zinachafua career
yangu kiukweli siwasemei wengine lakini kama unataka kuendelea na career
hii lazima ukae mbali na mambo hayo,” alisema Jihan. “kusema kweli sipo
kwenye mahusiano am really focused on my caree kwa sasa,”
Jihan
amesema anaamini ili afanikiwe ni lazima afanye kwanza kitu
kilichomsimamisha kwenye mitindo ndipo baadae afanya mambo mengine.
Mrembo
huyo anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya
urembo duniani Miss Universe ambayo yatafanyika mapema kwakani.
0 comments:
Post a Comment