Na sababu yenyewe ya kwa nini mke wake pamoja na mtoto wao mwenye umri wa miaka 10 kubakia katika jiji la New York,ni kwa ajili ya mwanao kumalizia masomo yake katika shule moja ya private iliyoko katika jiji la New York.Chanzo cha karibu kabisa na bwana Trump kililiambia gazeti la New York post kwamba"Melania yuko karibu sana na mwanae Barron na wamekuwa na ukaribu sana hasa wakati wa uchaguzi"."Kampeni za uchaguzi wa Marekani imekuwa ngumu sana na imemuwia vigumu sana kwake kwa sababu ya mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea mitandaoni hasa kuonekana kwa picha za utupu za mama ayake mtandaoni,kumemchanganya sana".Alisema
Hata hivyo uamuzi wao wa kubaki katika nyumba ya bwana Trump utaongeza changamoto nyingi sana za kiulinzi,katika mamlaka ya ulinzi ya siri ya Marekani(secret service) na kitengo cha polisi(Police departiment),kwa sababu nyumba ya bwana Trump iko katika maeneo ya ubize mwingi sana.Na wanachama wa mtaa huo wanaweza kuingia katika jengo hilo na kutoka kama wanavyotaka.Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilizungukwa na wapingaji wa matokeo pamoja na wanahabari wakiwemo polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.
0 comments:
Post a Comment