Na Sosy
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda awashukia askari
wa jeshi la polisi wanaokula rushwa na kunyanyasa wananchi na kuwataka watoe
majibu ya malalmiko hayo.
Paul Makonda amezungumza hayo leo alipokuwa Keko Wilayani ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku ndani ya Jiji la Dar es
Salaam ambapo alisimama kusikiliza malalamiko ya wananchi wa eneo hilo mara
baada ya kutoka kukagua kiwanda ya feniture cha Mwanalisa na kiwanda cha Gysum
.
Awali makonda alisimamisha msafra wake na kutaka kusikiliza
kero za wannchi kama ilivyo lengo la ziara hiyo ambapo alisimama mwananchi
mmoja alisimaana kueleza kuwa yeye aliahikukamatwa najeshi hilo mara baada ya
kuhoji utaratibu wa jeshi kukamata watu bila ya kosa.
Mwananchi mwengine liyejitambulisha kama mama saidi alisem
kuwa mtoto wake ambaye ni dereva bodaboda aliyekamatwa kwa muda mrefu bila ya kupewa
dhamani ilhali hana kosa nab ado askari hao wanadai rushwa ya shilingi laki nne
ikiwa tayari ameshawapa laki mbili lakini bado mtoto wake hajaachiwa na wala
hajapewa pikipiki yake.
Baada ya kusikiliza malalamiko hayo Makonda amesema kuwa
anataka majibu hapo hapo kutokana na kuwa amefutana na wahusika katika kila
idara ambapo kwa jeshi la polisi alikuwa yupo pamoja na kamanda wa Mkoa wa
kipolisi wa Temeke kamanda Mroto.
Kamanda Mroto akijibu hoja hizo amesema kuwa jeshi hilo lipo
katia kusimamia sharia na kwamba mtu yoyote atakayekwenda kinyume na sharia atawajibishwa
ikia pamoja ana baadhi ya askari polisi wasiokuwa .
Kamanda Mroto amesema kuwa hata wananchi nao wanatakiwa
wasivunje sharia kutokana na kuwa waendesha bodaboda wamekuwa wavunjaji
washeria hivyo wanapovunja sharia watawajibishwa
Amesem kuwa mwananchi yoyote atakayekutana na askari wenye
kutaka rushwa waende wawalipoti na waikubali kutoa rushwa.
Mwisho Makonda
amesema kuwa wananchi wafuate sharia hasaa waendesha bodaboda pia na kuwataka
polisi wanaokula rushwa wawajibishwe.

0 comments:
Post a Comment