MAKONDA
NA BASHIR NKOROMO, UBUNGO
Wakati imezoeleka kusikia kuwepo kwa wafanyakazi hewa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paull Makonda ameshangaa baada ya kubaini kuwepo barabara hewa ambayo ujnenzi wake umegharim mamilioni ya fedha katika kata ya Msigani, wilayani Ubungomkoani kwake.
Kuwepo kwa barabara hiyo kuliibuliwa miongoni mwa wananchi waliokuwa wakieleza kero zinazowakabili katika kata yao ya Msigani, Mkuu huyo wa mkoa alipokuwa akiwasiliza, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika mkoa wa Dar es Salaam.
kwa usimamizi wa mtendaji wa Kata hiyo, kwa baraka za halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, lakini cha kushangaza barabara hiyo ikaelezwa kuwa haipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Barabara (TANROADS) wala Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambayo ndiyo inayosimamia kwa kuwa kwa sasa bado Wilaya ya Ubungo haijawa na Halmashauri.
Ilielezwa katika mkutano uliofanyika kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa a Temboni Kata ya Msigani, kwamba barabara hiyo ni inayotoka Msigani kwenda Kinyerezi.
Kufuatia malalamiko kuhusu barabara hiyo, Makonda aliamuru Polisi kumsaka Mwenyekiti huyo wa mtaa na kumhoji pamoja na wale wote alioshirikiana nao katika kadhia hiyo..
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole (kulia), kuhusu mradi wa maji wa Kata ya Temboni Kata ya Msigani, alipokagua mradi huo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi wa papo hapo au wa baadaye katika wilaya hiyo leo.
Baadhi ya wananchi wakimweleza Makonda kero zao kwa njia ya bango alipokuwa kwenye mkutano kwenye Ofisi ya Mtendaji mtaa wa Temboni, Kata ya Msigani
Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole akitoa maneno ya utangulinzi kumkaribisha Makonda kuzungumzaa na wananchi
Mkazi wa mtaa wa Temboni, Moreen Gomba akitiririka kueleza kero wakati wa mkutano huo uliofanyika mbele ya Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, Kaya ta Msigani wilayani Ubungo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisikiliza kwa makini wakati wananchi wa Kata ya Msigani wakieleza kero zao kwenye mkutano aliofanya kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, leo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole.
Makonda akimhoji maswali Mtendaji wa Mtaa wa Temboni, Ramadhani Dilolo (kushoto), kuhusu kero zilizoelekezwa kwake na wananchi wakati wa mkutano huo
UZINDUZI MRADI WA MAJI KATIKA SHULE YA SEKONDARI GOBA MPAKANI
🔻
Makonda akizungumza kabla ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa na mfadhili katika Shule ya Sekondari Goba Mpakani
Makonda akizindua mradi wa maji katika shule ya sekondari ya Goba Mpakani, akiwa katika ziara hiyo, leo.
Makonda akimpongeza Polepole baada ya kuzindua mradi huo wa maji. Baada ya kuzindua mradi huo Makonda aliahidi kugharamia ujenzi wa visima vinane katika Kata ya Goba
MTAA WA MATOSA, KATA YA GOBA
Kijana akiwa ameshikiliza bango kufikisha kero kwa Makonda kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matosa kata ya Goba
Mkazi wa mtaa wa Matosa akifurahia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na Makonda katika mtaa huo leo
Makonda akimsilikiza kwa makini Polepole wakati akimshauri jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika mtaa wa Matosa
Makonda akienda kuizindua vyumba vya madarasa katika shule ya Matosa, Kata ya Goba wilayani Ubungo leo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizindua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Matosa, Kata ya Goba wilayani Ubungo
Makonda na Polepole wakisindikizwa na wananchi wakati akienda kuzindua ujenzi wa nyumba ya Walimu baada ya kuizndua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizindua ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo ya sekondari













0 comments:
Post a Comment