Mpemba na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kula njama za kufanya uhalifu na kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria.
Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Paul Kadushi, alisema kwa nyakati tofauti kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016, jijini Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara, watuhumiwa hao walitenda makosa hayo.
Mtuhumiwa huyo na wenzake Charles Mrutu (37), Benedict Kungwa (40), Jumanne Chima (30), Ahmed Nyagongo (33) na Pius Kulagwa (46) hawakutakiwa kujibu chochote na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba Mosi, mwaka huu itakapotajwa tena huku watuhumiwa hao wakirudishwa rumande.
Mwezi Oktoba mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini hapa, alimtaja Mpemba kwamba amekuwa akisikia habari zake kwenye taarifa za kuhusika na biashara hiyo haramu na kuwapongeza waliofanikisha kukamatwa kwake.
IFUATAYO NI HATI RASMI YA MASHITAKA YA WATUHUMIWA:
NA DENIS MTIMA/GPL
0 comments:
Post a Comment