Na Sosy
MWENYEKITI soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manspaa
ya Temeke Mukiwa Hassani hii leo ametoakaili yam waka baada ya kuomba kupigwa
risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kutuhumiwa
kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa
kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikilizakero zinazowakabiliwananchi ikiwa ni
siku ya pili ya ziara yake katika manispaa ya TEMEKE.
Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi
ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa DSM kutoa nafasi kwa wakazi wa mbande
hususani wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.
Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti
wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma
hizo ndipo alipotoa kauli hiyo.
Kufuatia utetezi huo ikamlazimu mkuu wa mkoa kutumiabusuara
ambapo akamuagiza mkuu wa wilaya ya TEMEKE kusimamia uundwaji wa uongozi wa
soko hilo haraka.
Mkuu huyowa mkoa pia ametumia ziara yake hiyo kutembela eneo kitakapo
jengwa kituo cha polisi katika kata ya chamazi ikiwa ni moja mikakati ya
serikali katika kupambana na uhalifu.
Lengo la ziara hiyo ni kusikiliza kero za wananchi.Makonda
aliytembelea Soko hilo kwa ajili ya kusikiliza hoja za wanachi hao, ambapo
baadhi ya wananchi walilimlalamikia mwenyekiti wa soko hilo kuwahujumu wananchi
kwa kukodisha vizimba vya kufanya biashara katika soko hilo kwa kiwango kikubwa
cha fedha ilhali hatoi stakabdhi ya malipo.
Hassani aakijibu hoja hizo amedai kuwa amezushiwa na kwamba
akikutwa na hatia apigwe risasi mbele ya RC Makonda


0 comments:
Post a Comment