![]() |
| ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA MTAA KWA MTAA |
JESHI Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke
limeanza operesheni ya tokomeza ‘Panya road’ kwa kufanya msako wa mtaa kwa
mtaa ili kukomesha makundi ya vijana wenye nia ovu ya kufanya uhalifu pamoja na uporaji, wizi kutumia silaha, na makundi mengine ya kihuni.
Operesheni hiyo itawashirikisha wenyeviti wa mitaa pamoja na
watendaji watakao ongozana na askari wa jeshi hilo kuwasaka vijana hao katika
mitaa mbalimbali ya Temeke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Giles Muroto
akizungumza na Wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na watendaji wa wilaya ya
Temeke amesema hali ya Usalama katika ukanda wa Temeke na Mbagala inatia shaka
hasa kutokana na vijana wadogo chini ya Miaka 18 kujihusisha na Uhalifu.
Amesema wananchi wasioshiriki ulinzi
shirikishi watachukuliwa hatua kali ikiwemo kutozwa faini ya Elfu hamsini
pamoja na kifungo cha miezi sita jela, huku wenyeviti wa mitaa wametakiwa
kuwatambua wakazi wao kinyume chake watakuwa matatani pindi uhalifu
utakapotokea katika mitaa yao.
Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Nasibu Mbaga
amewataka wenyeviti hao kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kuhusu suala la
ulinzi na Usalama ambapo pia Mkurugenzi wa TRA mkoa wa Temeke amewataka
watendaji kuhakikisha wanatoa Ushirikiano katika Ukusanyaji wa kodi za majengo.

0 comments:
Post a Comment