 |
| MWENYEKITI WA MTAA WA GONGO LA MBOTO AKITIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI MARA BAADA YA AMRI YA RC MAKONDA |
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gombo la Mboto Bakari Shingo
atiwa mbaroni na jeshi la Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za kukusanya
mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na
Halmashauri inavyoagiza, kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu
na kushirikina na wahalifu.
tuhuma hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni,
kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni
kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.
Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe
wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya
mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka
husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu
na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
0 comments:
Post a Comment