![]() |
RAIS MAGUFULI ALIPOKWENDA
KUMJULIA HALI
MZEE SITTA NYUMBANI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Astushwa na taarifa ya kifo cha Spika
Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta.
Mzee Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika
hospitali ya Technical University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa
matibabu tangu mwezi uliopita.
Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kufuatia kifo hicho.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam ambayo BLOG YA WANANCHI imetufikia Katika salamu hizo , Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Samwel Sitta na Taifa limempoteza mtu
muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.
“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na
tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika
ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.
“Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa
Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia
nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.
Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki
kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema
peponi, Ameni”

0 comments:
Post a Comment