RAIS MAGUFULI
Na Sosy
RAIS wa Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania John Magufuli, ameweka mikakati imara.Hayumbishwi kwa
kile anachokiiamini kuwa anafanya kwa ajili ya watanzania na sio maslahi yake.
Rais
Magufuli ameweka nadhiri ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi ambayo
anaitekeleza kwa kasi kubwa
Moja ya
mambo anayoyaamini kuwa yatasimamisha uchumi wa Tanzania nia pamoja na kujenga
viwanda nchini.
Katika kutekeleza
agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo
hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha
viatu na bidhaa za ngozi
Makubaliano
haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali
wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao
Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam.
katika
makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu
cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na kufunguliwa na Baba wa
Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pamoja na
kiwanda cha sasa PPF itajenga kiwanda kipya cha kisasa ambacho kitakuwa
kikisindika ngozi na kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi kwa kutumia mashine
za kisasa na teknolojia ya hali ya juu na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua
masoko ya viatu nchini na kuongeza pato la Taifa.

0 comments:
Post a Comment