Rapper wa kike Bongo mwenye swagga za hatari, Chemical amefunguka na kusema
yeye bado ni bikira (hajawahi kujigijigi tangu azaliwe).
Alisema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi
cha D’WIKEND CHATSHOW kinachorushwa kupitia Clouds TV.
“Sijawahi kuwa na mahusino na mtu yeyote,”
alisema.
“Siri ya kujitunza hadi leo hii kuwa bado nipo
hivi ni kutokana na jinsi ambavyo nimelelewa maana mara nyingi nyumbani huwa
tunaambiwa kuwa usifanye hivi na vile hadi uolewe, na mimi kwahiyo nimekuwa
hivyo nikawa naogopa,” aliongeza.
Hata hivyo Chemical amesema licha ya kuwa
bikira, hajawahi kujihusisha na mapenzi na wasichana wenzake (ulesbian).
0 comments:
Post a Comment