
Story
kuhusu uhusiano wa kimapenzi uliokuwepo kati ya rapa Young Dee ambaye
aliwahi kuwa na uhusiano na Video Queen Tunda waliyeacha baada ya
kutoelewana kupelekana polisi.
Baada
ya kuwepo taarifa kwamba Tunda ameachwa na mwanaume anayetajwa kuwa
alikuwa akimgharamia kwa kila kitu ikiwemo kulipia nyumba, kununua
magari na starehe zote alizokuwa akizifanya kila siku, ikaja kuonekana
ameanza kuwa karibu tena na Young Dee.
Young
Dee ambaye ameeleza kuwa yeye na Tunda wako vilevile kama mwanzo
hawakuwahi kugombana na ameamua kumsamehe Tunda kwasababu itakuwa kosa
kubwa endapo hatamsaheme wakati yeye pia ana makosa makubwa zaidi ya
hayo ya Tunda.
“Mimi
nilikuwa na matatizo yangu mengi sana hata kufika hapa tu nimesamehewa
sana vitu vingi katika watu ambao hawakutakiwa kusamehewa ni mimi ndio
mana nimeamua kumsamehe, kwa yote ambayo Mungu amenisamehe nisiposamehe
nitakua nakosea sana” – Young Dee
0 comments:
Post a Comment