![]() |
| KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI HODHI YA RASILIMALI ZA RELI (REHCO),MASANJA KADOSA |
Na Sosy
BAADA ya Serikali kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa reli ya Standard Geuge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza tayari inakamilisha reli ya ndani ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza adha ya foleni.
KaimMkurugenzi Mtendanji wa kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania REHCO Masanja Kadosa amesema kuwa serikali imetenga Trilion 1 kwa ajili ya ujenzi huo.
amesema kuwa ujenzi wa reli za ndani utakamilika Mwezi Desema mwaka huu.
"Kuna Mradi wa
kujenga reli mpya katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kwa ajili ya
treni za abiria ili kupunguza msongamano wa abiria na magari. Mradi huu uko
katika hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali chini ya kampuni ya
ushauri ya GIBB Engineering ya Afrika Kusini na kwamba inatarajiwa kukamilika
Disemba 2016,” alisema.
HATA
hivyo ujenzi wa reli ya Standard Gauge kutoka Jiji la Dar es Salaam kwa
awamu ya kwanza itaanza rasmi Disemba 6, 2016.
"Ujenzi wa
reli ya standard gauge umeshaanza lakini hatua iliyokuwepo haionekani, tenda
zimeshaanza kutangazwa,”alisema
Kadogosa wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Alisema ujenzi huo utaanza kwa awamu na kwamba
awamu ya kwanza inatarajiwa kuanzwa Disemba 6, 2016 wakati ya pili itaanza
Februari 15, 2016.
“Ujenzi huo
utachukua miaka mitatu kukamlika, ambapo utaleta manufaa kwa kizazi cha sasa na
kijacho. Pia utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutokana na kwamba litakuwa na
mabehewa yenye kilomita 2 ambayo sawa na ukubwa wa malori 300,” alisema.
Alisema wamiliki wa majengo yatakayo athiriwa
na ujenzi huo watalipwa fidia.
“Hifadhi ya reli
ina maana kwamba kila upande inaachwa mita 30, hivyo kama kuna nyumba
zitakazokuwa nje ya mita hizo zitatakiwa kubolewa wamiliki watalipwa
fidia,” alisema.

0 comments:
Post a Comment