MSHAMBULIAJI Saimon
Msuva wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, kwa mara ya kwanza
amezungumzia taarifa za Thomas Ulimwengu kuichezea timu hiyo.
Akijibu maswali ya mashabiki wa soka kwenye kipindi cha
KIKAANGONI kupitia Facebook East Africa Television, Msuva amesema iwapo Thomas
Ulimwengu atakuja kucheza timu ya Yanga, itakuwa ni jambo zuri kwao kwani
Ulimwengu ana uzoefu mkubwa, hivyo watajifunza kitu.
"Sijajua kama kweli atakuja, kama atakuja itakuwa
vizuri kwetu, Thomas Ulimwengu atatupa changamoto kwa sababu kuna vitu vingi
amejifunza huko Mazembe alikokuwa, hivyo itakuwa changamoto kubwa kwetu na kwa
timu pia", alisema Saimon msuva.
0 comments:
Post a Comment