Mwigizaji
wa bongo muvi kwa upande wa komedi Tausi Mdegela amesema, mara nyingi
akiwa sehem za matembezi, watoto wengi wanamkimbilia na wengine kutafuta
vitenesi ili wacheze wakidhani supastaa huyo ni mtoto mwenzao.Watoto
wengine wanakuwa wanawasumbua wazazi wao(mama zao) wawanunulie nguo kama
alizovaa Tausi. Tausi amesema anapenda sana watoto na muda si mrefu
anategemea kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu japokuwa hakusema
ni lini. Ameongezea pia mchumba ambae anatarajia kufunga nae ndoa ana
kimo kirefu mwenye kuweza kuzima taa wanapokuwa chumbani. Muigizaji
Tausi ameongea haya wakati anahojiwa na Dina Marios katika kipindi cha
uhondo E fm radio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment