Mkuu wa shule ya Academic International Tanzania Shyama Santhosh.
Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti juzi na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa China, Inder Jit Sagar.
Dar es Salaam.
Wanafunzi wawili wa Shule ya Academic International Tanzania, wameweka
historia katika mitihani ya mtalaa wa Cambridge baada ya kushinda nafasi
ya kwanza duniani kwenye masomo ya hisabati na kompyuta.
Harshvardhan
Babla amekuwa wa kwanza mtihani wa somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa
kidato cha tano, huku Abishek Sankaranarayanan akishika nafasi ya kwanza
katika somo la Hisabati kidato cha nne.
Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti juzi na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa China, Inder Jit Sagar.
Pia,
walimu wa masomo hayo; Thadei Mwinuka anayefundisha somo la Kompyuta na
Walter Mlowe wa Hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi.
Akizungumza
katika hafla maalumu ya kuwapongeza, mkuu wa shule hiyo, Shyama
Santhosh alisema wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule,
walimu na nchi.
“Huu
ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu na nchi, mtihani wa Cambridge
unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika
nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia hii
inaonyesha walimu wetu wapo makini,” alisema.
Source:- Mwananchi Blog

0 comments:
Post a Comment