Vigogo hao ambao
walitambulishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga waliamsha
shangwe kwa wabunge wa kambi ya upinzani, huku wabunge wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), wakiwa wamekaa kimya na wengine wakitabasamu.
Baada ya Bunge
kuahirishwa mchana, viongozi hao walitoka nje na kusalimiwa na wabunge
mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Newala, George Mkuchika, Mussa Ntimizi
(Igalula), Venance Mwamoto (Kilolo) ambao wote wanatoka CCM.
Serukamba ni moja ya
vijana watiifu kwa Lowassa, ambaye kwa miaka kadhaa, alikuwa akimuunga
mkono na wakati wote wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM katika
kinyang’anyiro cha kuwania urais mwaka 2015 alikua mstari wa mbele.
Taarifa zilizojiri
katika mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa, sababu iliyomfanya Serukamba
amkimbie Lowassa ni kuogopa taarifa kumfikia Rais Dk. John Magufuli,
ambapo wanaCCM waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa ndani ya chama hicho
hawaaminiki katika Serikali ya awamu ya tano.
Katika msafara huo,
Lowassa na Sumaye walikuwa wameandamana na wajumbe wenzao wa Kamati Kuu
ya Chadema ambao ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Profesa
Abdallah Safari na waziri wa zamani wa Serikali za awamu ya pili na
tatu, Arcado Ntagazwa.
Chanzo-Mtanzania
0 comments:
Post a Comment