Mfalme wa rhymes 2004, Afande sele kaelezea hisia zake kwa msanii wa hip hop Darasa, Afande seleanasema kwamba wapo madogo zangu wengi kwenye game lakini umuhimu wa pekee nampa Darasa.
Kauli ya Afande sele inakuja kufuatia mzunguko wa ngoma za Darasa na jinsi alivyoleta kitu kipya kwenye rap.
Afande sele anaamini Darasa ni msanii anaye tumia akili sana “yoyote anaye tumia akili katika mambo yake anafikia malengo” Afande sele anaamini Darasa amekuja kufanya mapinduzi na kuiaminisha jamii kwamba hip hop haijafa, aidha katumia fursa hii kuwaambia wale wanaofananisha muziki wa hip hop na singeli kuacha mara moja kwasababu hip hop na singeli ni miziki yenye tamaduni mbili tofauti.
0 comments:
Post a Comment