Staa wa soka wa kimataifa mwenye uraia wa Tanzania Mbwana Samatta ametoa ya moyoni kuhusu mashavu anayopata kwenye ngoma nyingi za Bongo Fleva siku za karibuni.
Akipiga story na Perfect255 Mbwana Samatta ameonyesha ni kiasi gani anajisikia furaha baada ya kusikia akitajwa katika ngoma kama “Muziki” yakwake Darassa na hata “Kokoro” ya Rich Mavoko na Diamond Platnumz.
“Wasanii wakubwa kama hao wanapokutaja kwenye nyimbo zao ni jambo la kujivunia, ni swala zuri sana na nimejisikia poa, nimejisikia faraja. Nimeona kumbe kuna kitu nafanya na wao wanakipenda.” Alisema Mbwana Samatta.
Samatta pia hakutaka kuzificha hisia zake juu ya mapokeo yake katika ngoma hizo na kudai kuwa hizo ni ngoma zake bora kabisa na ndizo ambazo anatumia muda mwingi sana kuzisikiliza pindi awapo nyumbani au hata aendapo kwenye mechi.
Unaweza kuplay hii video hapa chini ili kumsikiliza mkali huyo wa soka akifunguka mwenyewe kiufafanuzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment