Jumamosi ya dec 17 2016, Alikiba kakwarua tuzo nyingine ya best celebrity player pande za Uganda.
Ulikua mchezo wa soka wa hisani kwajili ya kuchangia mfuko wa wamama wajawazito unaofahamika kama Dorah foundation.
Mchezo huo ulihusisha mastar mbali mbali, team ya The celebrity white team aliyochezea Alikiba iliibuka na ushindi wa 4-1 huku Alikiba akitupia goli la pili.
Katika mchezo huo wa aina yake alionekana pia mchezaji aliyewahi kutamba kwenye team za Yanga na Simba, namzungumzia Okwi ambaye alicheza team moja na Alikiba.
Baada ya mchezo huo kumalizika, king Kiba from +255 alijishindia tuzo yake ya best celebrity player

0 comments:
Post a Comment