Thursday, December 15, 2016

11243089_369824013207924_1262238902_n
Vita kati ya Mary J. Blige na aliyekuwa mume wake na meneja, Martin “Kendu” Isaacs, vimechukua sura mpya.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, muimbaji huyo wa ‘No More Drama’, ana mshutumu Isaacs kwa kugoma kumkabidhi baadhi ya mali zake yakiwemo magari ya kifahari, tuzo ya Grammy na nyingine.Blige, 45, anadai kuwa Isaacs anashikilia magari yake aina ya Mercedes C300 na SL550, na pia alimtapeli $420,000 wakati alipokuwa meneja wake.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2003 na kupeana talaka mwezi July. Isaacs ametaka Blige amhudimie ikiwemo $130,000 kila mwezi kwaajili ya matumizi yake mbalimbali.
Mbali na hilo, Msanii huyo wa RNB Queen Mary J. Blige alidropisha video yake mpya mwezi Nov mwaka huu ya wimbo wake “Thick of It,” kutoka kwenye album yake ya Strength of a Woman.

0 comments:

Post a Comment