Wednesday, December 14, 2016

Tulibakiwa na viporo viwili tu vya mechi katika ligi ya EPL ilikukamilisha idadi ya mechi 15 ambazo zimechezwa na timu zote za ligi hiyo. Mechi iliyozikutanisha Arsenal na Everton huku Leicester city iliwakaribisha Bournemouth.
Arsenal walifanikiwa kumiliki mpira muda wote na kuanza vyema kwa kufanikiwa kuliona goli la Everton katika kipindi cha kwanza cha mchezo. Alexis Sanchez’ alifanikiwa kucheka na nyavu baada ya kuutendea vyema mpira wa adhabu alioupata.M


Mipango ya Arsenal haikufua dafu mbele ya Everton na kujikuta wakitoka vichwa chini kwa kutundikwa goli mbili wao wakibakiwa na moja. Mchezo ulikuwa na vurugu sana jambo ambalo liliwapa wakati mgumu Arsenal na kujikuta wanashidwa kuzilinda nyavu zao.

0 comments:

Post a Comment