KING of the best melody Christian Bella ametamba kuwa yeye ndiye atakayeibuka kinara kwenye shindano liloandaliwa na Mkuu wa Dar es Salaam Paul Makonda litakalo mkutranisha yeye na mkongwe wa muziki nchi Banana Zoro.
RC Makonda wiki moja iliyopita aliwataka wasanii hao wawili kuandaa
show ya pamoja ili washindane kuimba live na mshindi atampatia tsh
milioni 50.
Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella, amedai hana shaka na
pesa hizo kwani anajua atamshinda Banana na kuondoka na kitita kicho
kikubwa cha pesa.
“Tunamshukuru Mh Paul Makonda ni wazo zuri sana kwa kutujali vijana,
kwa kujali vipaji na kuvithamini,” alisema Bella. “Kwahiyo sisi
tunaiandalia mazingira ili kuangalia itakuwaje kwa sababu tunatakiwa
kuwa serious sana lakini tumeshapanga itakuwa mwezi wa pili au wiki ya
mwisho ya mwezi Januari,”
Aliongeza, “Kwa upande wangu mimi sasa najiandaa, mimi sitaruka
sarakasi bali nitaperform vizuri ngoma zangu zote kali, niimbe zaidi,
nitafanya performance ya hasira ili nipate hiyo hela. Lakini mimi
naamini hiyo hela niyakwangu hata kama Banana Zorro ni mkali na anaimba
vizuri, mkongwe, kipaji lakini naamini mimi nitachukua hiyo hela,”

0 comments:
Post a Comment