Baadhi ya watumishi wa Multichoice wakiwa na baadhi watoto yatima kituo cha Al madina.
Multichoice Tanzania imeonyesha namna ambavyo jamii inaweza kukumbukwa baada ya kutoa misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Al Madina cha Tandale jijini Dar es Salaam, leo tarehe 22/12/2016.
Timu nzima ya Multichoice Tanzania, ilitua katika kituo hicho ikiongozwa na Meneja Mtendaji, Maharage Chande na kupokewa na mlezi wa Al Madina Children Home, Bi Kuluthum Yusuph,watoto hao walioonekana kuufurahia ugeni huo.
Bwa Chande ameahidi kuendelea kukisaidia kituo hicho. "Sisi kama Multichioice Tanzania tunaahidi kuendelea kutoa japo kidogo tutakachokuwa tunakipata ili watoto hawa wasijihisi kutengwa na jamii,"
Meneja utendaji Bwa, Chande pichani akiwa na mlezi wa kituo Bi, Kuluthum
Naye mlezi wa kituo hicho, Kuluthumu Yusuf katika hali ya kushukuru alisema: "Nawashukuru sana Dstv kwa kuendelea kutusaidia, kutoa ni moyo na wanauonyesha kwetu. Tunaomba na makampuni mengine yaige mfano wao yajitokeze kutusaidia hata yunifomu za hawa watoto."
Mwezi wa saba DSTV walitoa charahani ili kifungue mradi wake wa kushona nguo ili kujiingizia kipato cha kuwezesha kuendesha shughuli ndogo ndogo za hapo kituoni na hizo ndizo picha za maendelea ya mradi huo.
Kati ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na unga wa ngano, sukari, sabuni, mchele na vitu vingine mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.
Multichoice kupitia DSTv wamekuwa wakionyesha chaneli mbalimbali ambazo ni maarufu nchini na Afrika nzima kama SuperSport upande wa michezo, M net, Movie Magic na nyingine upande wa filamu lakini kuna zile maarufu za taarifa ya habari kama CNN, Al Jazeera, BBC na nyingine nyingi zinazohusisha elimu na burudani.
0 comments:
Post a Comment