Friday, December 30, 2016

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ni miongoni mwa wasanii wa Hip Hop ambao wamefanya vizuri sana kwa mwaka 2016, Kwani mbali na nyimbo zake kali kama SumuRohoBongo Hip Hop na Walk it Off pia amefanikiwa kutumbuiza karibia matamasha yote makubwa yaliyoweza kutikisa bongo.

Fid Q
Sasa endapo ukikutana na Rapa huyo na ukamuuliza ni msanii gani umeona kwa mwaka 2016 anastahili kupata Tuzo ya Hip Hop? Basi Rapa huyo mkongwe Fid Q, asingesita kufunguka na kuwataja Marapa wawili, ambao ni Wakazi na Nikki Mbishi kwani yeye anaamini wanavipaji na wanatoa ngoma kali kila kukicha ingawaje bado mashabiki hawatoi Sapoti ya kutosha.
Kupitia EA Radio Fid Q alisema “Kiukweli napata wakati mgumu sana lakini naona, napenda juhudi sana za Wakazi anajituma lakini kuna msanii anaitwa Nikki Mbishi, amekuwa akitoa ngoma nyingi kali lakini watu wameamua kulala tu juu yake.
Aliongeza, Nafikiri  2017 mnahitaji kidogo pia kuwazingatia watu kama Nikki Mbishi kwa sababu wanafanya vizuri, na unapojua wewe ni msanii na unafanya vizuri na unaona watu hawana mpango na wewe, kidogo inaweza ikaku-frustrate na kuleta shida mbeleni. Kwa hiyo tujaribu kuangalia na kuzingatia jinsi gani tunaweza kubeba vipaji vya wenzetu wengine ili tuweze kuinyanyua hii platform na kulitangaza taifa vyema”.

0 comments:

Post a Comment