Rapper Nay wa Mitego amefunguka kuhusu tetesi zinazovuma kumuhusisha kuwa katika maelewano ambayo sio mazuri na aliyekuwa producer wake katika studio yake ya Free Nation Mr T-Touch.
Ni alhamisi iliyopita kwenye XXL ya Clouds FM wakati akitambulisha ngoma yake mpya ya “Sijiwezi” ndipo alipokutana na swali kutoka kwa BDozen kuhusu yeye ana matatizo gani na aliyekuwa producer wake licha ya kumtengenezea hits kibao.
“Mimi na Mr T wala hatuna matatizo, sisi ni familia, kuna vitu tu ambavyo havijakaa sawa lakini kwangu mimi bado namchukulia kama bado mwanafamilia. Sijawahi kumuongelea vibaya Mr T-Touch labda yeye anavyoongea huko lakini mimi sina tatizo naye kabisa.” Alisema Nay wa Mitego.
0 comments:
Post a Comment