
mshambuliaji wa kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji amezisikia ngoma ya darasa aliyotajwa "Muziki na Maisha na ngoma ya Rich Mavoko Kokoro amesema haya kuhusu kutajwa kwake.
baada ya jina lake kutajwa kwenye nyimbo za wasanii hao amesema kwake ni heshima kubwa kuwepo kwenye nyimbo za wasanii na inaonesha ni namna gani wanavyothamini kitu anachofanya.
Star huyo wa soka la Tanzania ametajwa kwenye nyimbo mpya za Darasa (Muziki) na Rich Mavoko (Kokoro) ambazo kwa sasa zinafanya vizuri kwenye soko la muziki.
“Wasanii wakubwa kama hao wanapokuzungumzia na kukutaja kwenye nyimbo zao ni jambo la kujivunia, ni suala zuri na nimejisikia poa. Nimejisikia faraja yani moyo wangu umekuwa baridi, kumbe kuna kitu nafanya wanakipenda kwa hiyo fresh kabisa,” amesema Samatta amabye ame-assist goli moja lililofungwa na Heynen katika mchezo wa Europa League dhidi ya Sassuolo uliomalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 2-0 ugenini.
“Yani hizo ndio ngoma zangu kwa sasahivi zilizonishika kwa kiasi kikubwa, nasikiliza muda mwingi hata nikiwa naenda kwenye game nasikiliza nazisikiliza hizo ngoma.”
0 comments:
Post a Comment