Chris Brown ndani ya Headline mpya na mwanadada Krista Santiago.
Baada ya kuwa kimya muda mrefu bila kupata mainfo yeyote yale kuhusu maisha ya Chris Brown kwenye upande wa mahusiano, uvumi mwingine ambao umetawala kwa sasa ni kwamba Chris Brown anatoka kimapenzi na model kutoka New Jersey anayefahamika kama Krista Santiago na uvumi wao ulianza muda mrefu tangu mwezi October.
Uvumi kuhusu mahusiano yao ulianza kwa mara ya kwanza pale Chris Brown ameonekana akiwa na mwanadada Krista kipindi cha Halloween, mwezi uliopita nao yalikuwa yaleyale baada ya Chris Brown kuonekana tena na Krist wakila bata.
Sasa Good Newz nyingine ni kwamba wiki iliyoisha, Chris Brown ameonekana kwenye Instagram akilike picha ya Krista pindi anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, hata hivyo Krista aliposti picha akiwa amepewa zawadi na Chris Brown kwenye Snapchat na baada ya muda akaifuta.




0 comments:
Post a Comment