Wednesday, December 21, 2016


Ice Prince anahitaji umwekee “caption” kwa picha zake na Vanessa Mdee.
Baada ya kuachia Album yake ya “Jos to the World” ambayo imebeba ngoma takribani 19, ndani ya Album hiyo Ice Prince amemshirikisha mrembo wetu Vanessa Mdee katika Abum hiyo kupitia ngoma ya “No mind Dem”, Kama hujapata kuusikiliza huu wimbo fahamau kwamba ni bonge moja la ngoma ambalo ndani unakutana na fleva za kibongo kutoka kwa mtoto mzuri Vee Money.

Good Newz inaonekana kuna ujio wa video ya “No Mind Dem”, Kupitia kurasa ya Ice Prince amekuwa akiposti picha akiwa na Vanessa Mdee huku akiweka Hashtag ya “NoMindDem” ambapo inaonyesha video imeshaiva bado kupakuliwa tu kwa mashabiki, ila Ice Prince bado anajambo moja kutoka kwako anahitaji kupatiwa Caption.





0 comments:

Post a Comment