Saturday, December 31, 2016

Leo December 30, 2016 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam limetoa taarifa ya oparesheni mbalimbali zilizofanywa ili kuhakikisha kuwa tatizo la uhalifu na wahalifu wanadhibitiwa na kutokomezwa kabisa kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 hadi Desemba 2016.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM, Kamishna Simon Sirro amesema oparesheni zilizofanyika kwa kutumia vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM likiwemo Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha, Kikosi cha Mbwa na Farasi, kikosi cha Kuzuia Wizi wa Magari, Kikosi cha Askari Kanzu, Kikosi cha Intelejensia, Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Ng’ombe, kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya na Kikosi cha Kuzuia ghasia( FFU) zimeweza kuleta mafanikio mbalimbali kama ifuatavyo:-
  1. Idadi ya watuhumiwa 7625 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kupatikana na bhangi kilogramu 2843 na gramu 78
  2. Jumla ya watuhumiwa 269 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya Madawa ya kulevya  ya aina  mbalimbali kama ifuatavyo: Cocaine kilo 3 gramu 255  na  Heroine  kilo 1 gramu 654
  3. Pia pombe haramu ya Gongo jumla ya lita 8547, mitambo 34 na watuhumiwa 5627 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
  4. Watuhumiwa 126 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya Madawa ya kulevya aina ya Mirungi kilo 75  na gramu 254  
  5. Jumla ya Silaha 67 na risasi 1076 za aina mbalimbali zilikamatwa pamoja na watuhumiwa 52 na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha/UGAIDI.
  6. Jumla ya wahamiaji haramu 105 toka mataifa mbalimbali walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA JAN-NOVEMBA 2016 UKILINGANISHA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2015
S/NO.KOSAMWAKA 2015MWAKA 2016ONGEZEKOPUNGUZOASILIMIA
1.MAUAJI3272913611%
2.KUBAKA9721030586%
3.KULAWITI3103837323.5%
4.WIZI WA WATOTO2619727%
5.KUTUPA WATOTO27151244%
6.UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA2041277737.7%
7.UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU118187430726%
8.UVUNJAJI567753553225.7%
9.WIZI WA MAGARI3923217118.1%
10.WIZI WA PIKIPIKI2644219145317.1%
11.WIZI WA MIFUGO1971633417.3%
Sababu za  kuongezeka  au kupungua kwa  matukio haya  kumetokana  na juhudi za Polisi Kanda  Maalum kuzuia na kupambana na uhalifu kwa kufanya doria  pamoja na misako mbalimbali iliyopelekea kukamatwa kwa wahalifu wa makosa mbalimbali kwa   kushirikiana na   raia wema  kwa kutupatia   taarifa za siri ili kugundua  makosa ambayo  yanakera  jamii. Jumla ya wahalifu 13,626 walikamatwa na kufikishwa mahakamani

0 comments:

Post a Comment