Naanza kuona kama mzimu wa Pogba unaanza kumvaa Kanye West, yale mambo ya kubadilisha nywele na kuweka marangi rangi kichwani.
Baada ya kutuonyesha blonde staili yake ya nywele, Kanye ameamua kuphotoshop nywele zake kwa kuongeza rangi ya nyekundu na machungwa flani hivi, staili hiyo ilishuhudiwa siku ya jumatatu baada ya kutoka jumba la Cinema huko L.A
Kama utakumbuka Dec 8, pindi Kanye ameonekana kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Hospitali, mashabiki walianza kuona mambo ya tofauti kwa Kanye akiwa watofauti katika nywele zake na staili yakee ya Blonde.
Kikubwa ambacho bado mashabiki wa Kanye wanachoamini ni kwamba Familia ya Kardashians ndio inampelekea kuwa hivyo na hivi baada ya tetesi kibao kusambaa kuwa Kanye na Kim wako mbioni kuachana basi ndilo jambo ambalo linazidi kumvuruga rapper huyo.
0 comments:
Post a Comment