Friday, December 16, 2016




Siku kama hii ya leo miaka 18 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'...
Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi. Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho. Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa...


Miaka 67 iliyopita katika siku kama ya leo harakati ya kupigania uhuru ya watu wa Cyprus ilihitimisha ukoloni wa Waingereza kisiwani humo. Kisiwa cha Cyprus kilichoko katika Bahari ya Miditerranean kiliwekwa chini ya utawala wa Kiothmania katika karne ya 16. Mwaka 1925 Uingereza ilikiunganisha kisiwa hicho na makoloni yake na tangu wakati huo kulitokea mapigano baina wakazi wa kisiwa hicho yaani Waturuki na Wagiriki. Hatimaye Cyprus ilipata uhuru mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Wagiriki huku Waturuki wa kisiwa hicho wakidhibiti eneo la kaskazini la nchi hiyo.

Na siku kama ya leo miaka 252 iliyopita alifariki dunia huko Karbala, Iraq faqihi, mpokezi wa hadithi, mhakiki na mwandishi maarufu wa Kiislamu katika karne ya 12 Hijria Sheikh Yusuf Bahrani. Alijifunza elimu ya msingi kwa baba yake na baadaye alielekea Bahrain na Makka kwa ajili ya kupata elimu ya juu. Baadaye alielekea katika mji wa Fasa kusini mwa Iran ambako alianza kufundisha na kuandika vitabu. Wakati huo alianza kuandika kitabu chake kikubwa zaidi cha fiqhi kinachoitwa "al Hadaiqun Nadhirah". Mwanazuoni huyo ameandika vitabu 32 katika taaluma mbalimbali vikiwa ni pamoja na "Anisul Musafir" na "Jalisul Khawatwir.''

Blog ya wananchi kila siku itakuwa ikikuletea historia ya watu maarufu na mashuhuri duniani kutokana na tarehe au matukio waliyofanya.

0 comments:

Post a Comment