Friday, December 16, 2016


Kuanzia Ijumaa iliyopita ishu iliyokuwa ikitrend zaidi kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu rapper Young Dee kumkataa mtoto ambaye amezaa na msichana afahamikae kama Mamisa.

Picha liliendelea baada ya Young Dee kumkubali mtoto huyo na kuahidi kutoa huduma zote kama Baba. Haikuishia hapo tu, mapicha picha kuhusu wasichana ambao wamewahi kusikika kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Young Dee (Tunda na Amber Lulu) kufananishwa na mzazi mwenzake huyo na Young Deendio kitu ambacho kili trend kinoma noma wiki hii nzima.
Hadi kupelekea mrembo Tunda kutoa POVU lisilo la polepole katika page yake ya Instagram na kulaani vikali kitendo cha yeye kufananishwa na wasichana hao wenzie.

Hakuwahi kusikika popote mrembo Mamisa kuzungumzia suala hilo, lakini leo U-Heard ya XXL imempata exclusive na kafunguka mengi sana baada ya Young Dee kumkubali mtoto wake.
Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mahaba moto moto baina ya wawili hao yamerejea kama kawa na Young Dee yupo katika mipango ya kumchukua kabisa bibie Mamisa na kuishi naye ili wamlee mtoto wao.
Ubuyo kamili nimekuwekea hapa chini kwenye video hii, bonyeza play kumsikiliza Mamisa ambavyo anatuma ujumbe kwa kina Tunda kuhusu Young Dee.

0 comments:

Post a Comment