Alisikika jana kwenye U-Heard ya XXL Q Chief akitoa malalamiko kuwa wimbo ulioachiwa hapo awali haukuwa rasmi bali ni demo ambayo ilivujishwa na producer ambaye alikuwa akiishughulikia kazi hiyo hapo awali.
Kutokana na kukua kwa teknolojia na kusababisha wimbo huo kusambaa zaidi hapo jana tofauti na matakwa ya Q Chief, mkali huyo ameamua kuiachia rasmi original version ya wimbo huo.
Akipiga story na Perfect255 Q Chief amedai kuwa hakuwa na jinsi tofauti na kuiachia tu ngoma hiyo ukizingatia kwamba Demo ya ngoma hiyo ilikuwa imekwisha sambaa kwa kiasi kikubwa sana.
“Sikuwa na jinsi, kama imeshachuja me nimeona hapa hapa tu niiachie, kwasababu huyo mtu hakuwa na nia nzuri. Me nimeamua tu iende kwa sababu i have no option. Cha kuwaambia mashabiki zangu ni kwamba ile ngoma ya kwanza haikuwa original version, na hivyo wakitaka original version waingie Mkito wataipata huko.” Alisema Q Chief.
Unaweza kumsikiliza mkali huyo akifunguka kirefu zaidi kuhusiana na suala hilo kwa kuplay hii video hapa chini
Kama unataka kuidownload hiyo original version ya ngoma hiyo bonyeza hapa chini
0 comments:
Post a Comment