Watengezaji wakubwa wa simu za mkononi TECNO
Mobile na Klabu ya ligi ya Uingereza, Manchester City leo wanasherehea uzinduzi
wa ushirikiano wa kimataifa kwa miaka kadha.
Kama mshirika rasmi wa Klabu
ya mpira ya Manchester City, TECNO Mobile itashirikiana na klabu hiyo kukuza
mikakati ya masoko na matangazo ya kampeni sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo
bara la Afrika ambapo TECNO tayari inatambulika kama kinara wa soko la simu za
mkononi.
TECNO ambayo ni sehemu ya Transsion Holdings,
kwa mara ya kwanza ilianzishwa nchini China na kwa miaka kumi iliyopita imekuza
umaarufu wake katika masoko tofauti zaidi ya 40 yanayochipukia ambako mashabiki
wa Manchester City wapo na wanaendelea kuongezeka kila siku.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa ushirikiano huo
wa kimataifa uliofanyika kwenye kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya
vijana, Afisa Mkuu wa Biashara wa City
Football Group Tom Glick alisema“Tunafurahi kuwakaribisha TECNO Mobile
katika mkusanyiko wa ushirikiano wa kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko
ya nyumbani kunaendana na namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia
kushirikiana nao kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote.
Stephen
Ha Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile akizungumza
katika uzinduzi katika kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha
Manchester City aliongezea:
“Tunashukuru sana kushirikiana na klabu yenye
mafanikio na inayojulikana ya Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa
muda mrefu katika michezo kwa hali ya juu”
“Kwa kuwapatia wateja wetu uzoefu wakufurahia zaidi
simu bora isiyolinganishwa na nyingine ni kipaumbele cha juu kwa TECNO Mobile
na tunaona ulinganifu mwingi mno na Manchester City tukiangalia mkazo wao
wanaoweka katika kuwapatia mashabiki wake uwezo wa kufurahia utofauti wa
kipekee kwa njia ya mtandao.
“Tunafuraha kujiunga na timu yao na tunasubiri
kwa hamu kuanzisha ushirika huu pamoja."

0 comments:
Post a Comment