Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Mtanzania Idris Sultan amepata shavu la kuwa host wa Tuzo kubwa za Fashion za Abryanz Style & Fashion Awards zinazotarajiwa kuhappen weekend hii huko nchini Uganda.
Perfect255 imepiga story na mkali huyo na kutaka kujua alijisikia vipi baada ya kupata shavu hilo ikiwa hizo ni tuzo kubwa sana barani Africa, ni vigezo gani ambavyo jamaa wametumia mpaka kumuona kuwa yeye anastahili nafasi hiyo.
“Namshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hii, Katikati ya mwezi November walinipigia simu na kuniambia kuwa wananifikiria katika mchongo huo, lakini sikutaka kuweka wazi kutokana na maneno maneno ya wabongo.”
Idris Sultan amevitaja vigezo zaidi ya vitatu ambavyo waandaaji wa tuzo hizo waliviangalia na kuamua kumpa shavu hilo. Unataka kuvijua vigezo hivyo? Play hii video hapa chini kumsikiliza yeye mwenyewe Idris Sultan akifunguka mwanzo hadi mwisho.
0 comments:
Post a Comment