Waasi wa Syria na wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakijaribu kuchukua mji wa A-Bab kutoka IS
Marekani imetaja madai hayo kutoka Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kuwa imeisaidia IS, ni ya Upuzi
Msemaji wa serikali Mark Toner amesema madai hayo hayakuwa na msingi.
Kiongozi wa Urusi alisema kuwa ana idhibati tosha iliyoonyesha Marekani imetoa msaada kwa makundi ya KiKurdi ya YPG na PYD. Wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakipigana kuiondoa IS kutoka Kaskazini mwa Syria.
"Wamekuwa wakitushtumu tunaisaidia Daesh," bwana Erdogan alisema kwenye kikao cha waandishi wa habari mjini Ankara, akitumia jina mbadala la IS.
"Sasa wanayasaidia makundi ya kigaidi yakiwemo Daesh, YPG, na PYD. "Ni wazi kabisa, Tuna idhibati tosha iliyothibitishwa, pamoja na picha na hata video."
Wanajeshi 37 wa uturuki wameuawa katika oparesheni iliyoanzishwa mnamo Agosti kuwaondoa wanamgambo wa IS na wapiganaji wa Kikurdi kutoka eneo maalum lililoko karibu na mji wa al-Bab, ulioko kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na makundi ya Ki Kurdi nchini Syria lakini Uturuki inasema pia wanahusishwa na Chama cha wafanyikazi wa Ki Kurdi, (PKK), kilichokuwa kikiendesha juhudu za mapinduzi ndani ya Uturuki kwa muda mrefu.
Aidha, muungano unaowakilisha makundi ya waasi na upinzani nchini Syria, umeyarai makundi hayo kushirikiana na juhudi zinazoendlea ili kufanikisha maafikiano ya kusitisha mapigano.
Lakini Riad Hijab, Mjumbe wa kamati ya majadiliano ya amani (HNC), amesema kamati hiyo, haijaalikwa kwenye kongamano lililopendekezwa na Urusi kufanyika Kazakhstan.
Hijab amesema mikakati ya kukuza uaminifu zinahitajika ili kuunda jukwaa la mazungumzo ya mabadiliko ya kisiasa anayosema yanastahili kufanyika mjini Geneva na kudhaminiwa na UN.

0 comments:
Post a Comment