Kila shabiki wa ngumi anatamani kuona Conor McGregor na Floyd Mayweather wakizichapa kwa ajili ya kumaliza mzozo wa maneno wanayotambiana...
Sasa Floyd Mayweather ametoa mchongo kwa mashabiki zake kwa kuwataka watafute Caption kubwa kuliko ambayo wataitumia katika video ambayo ameiposti katika kurasa yake ya Instagram ambayo inamwonyesha Conor McGregor akikubali kushindwa baada ya kupigwa kabali na mpinzani wake Nate Diaz na kukubali kuonyesha “Tapout.”
Conor McGregor ni moja ya mabondia wanaotishia sana katika ulingo wa Ultimate Fighting Championship (UFC), Picha linaanza muziki wa hawa jamaa sijui utakuwaje ukicheki kila mmoja anamkwanja wa kutamba na skills za kinyama katika maswala ya ngumi.
Kilichobaki ni kusubiri kuona nani atalala kifo cha mende kwenye mzozo huu..

0 comments:
Post a Comment