Saturday, December 10, 2016

15251569_361647034212127_9082072607863341056_n
Miss Tanzania 2016, Diana Edward amejikusanyia sifa nchini kwa jinsi alivyoweza kujichanganya na mamiss wengi waliopo nchini Marekani kwaajili ya shindano la Miss World. Kwa muda mfupi ameweza kupata marafiki, Miss Hondurus na Mexico wakiwa karibu naye zaidi.

Pamoja na kujichanganya nao vyema, Diana amewatambulisha warembo wake kwenye muziki wa Singeli na wanaonekana kuufurahia. Kupitia Instagram, Diana amepost video mbili zikiwaonesha, Miss Hondurus, Kerelyne Campigoti Webster na Miss Mexico, Ana Girault wakiucheza wimbo wa Man Fongo, Hainaga Ushemeji.
Video Player
00:05
00:10
Kwenye Instagram Girault ameandika: Learning new songs 😂😂😂👏🏼 maaaaambo! #MissWorld #MissMexicogoestoWashington.”
Video Player
00:00
00:09
Shindano la Miss World 2016, ambalo mwaka huu ni la 66, litafanyika December 18, kwenye ukumbi wa MGM National Harbor huko Oxon Hill, Maryland, Marekani. Hii ni mara ya pili shindano hilo linafanyika nchini humo.

0 comments:

Post a Comment