Awaomba Wananchi Na wadau wengine kuunga Mkono
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amelitaka jiji la Mbeya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi kukamilisha madarasa 10 ili wanafunzi 352 ambao Matokeo yao yamezuiliwa kutokana na kukosekana kwa vyumba vya madarasa

Hayo ameyasema Leo wakati wa kikao maalum na madiwani, watendaji wa kata na mitaa, wakuu wa idara , wajumbe wa bodi za Shule na wakuu wa Shule wa Shule ambazo zina upungufu wa madarasa
Amewataka kwa pamoja kujielekeza katika kuhakikisha madarasa hayo tanaka milima mapema mwezi januari ili wanafunzi hao waweze kuingia kidato cha kwanza

Ana imani ukamilishaji utawezekana kwakuwa madarasa hayo yapo ktk hatua YA upaauaji na ameshukuru jiji kwa kutoa sh 2.000,000 kwa kila darasa ili kuchangia umaliziaji

Amesema kushindwa kukamilika kwa ujenzi huo ni aibu kwa viongozi , watendaji na yeye mwenyewe hivyo nguvu YA pamoja inahitajika kukamilisha madarasa hayo



0 comments:
Post a Comment