Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia k akipokea gari la wagonjwa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 160 ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika ziara yake ya siku kumi aliofanya mkoani Dar es Salaam iliyokuwa na lengo la kusikiliza na kujibu kero za wananchi ilioambatana na kauli mbiu ya Dar mpya.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi hundi Wachungaji wa kanisa la AIC Tanzania.
Makonda amesema kuwa anatimiza ahadi zake kwa wahusika kama ifuatavyo Sober house kigamboni kwa kuwapa jiko la gesi, mitungi 2,king’amuzi televisheni moja ya nchi 49 na magodoro 50 pia ameweza kutoa zawadii ya pikipiki kwa watendaji wa ofsi yake kwa kuwapa morarli ya kazi pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mivinjeni kata ya buguruni.
Aidha mkuu wa mkoa ametoa zawadi kwa watumishi wane ambao ni Dr.Grace Magembe,mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mruto kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke,Edward Otieno katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji na Aron Joseph Mkkurugenzi uendeshaji wa DAWASCO.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mifuko ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya St Joseph Goba , Sister Caroline Kokutekana, kama sehemu ya kutimiza ahadi yake wakat wa mahafali ya shule hiyo.
Msaada mwingne alitoa mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mabati 2000 kwa ajili ya sekondari ya Jeshi ya jitegemee na shule ya msingi Annex Mbagala mabati 1000 na shule ya msingi ya katoliki kupewasaruji mifuko 1000 .
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akikabidhi zawadi tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi la Wananchi mara baada ya kufanya vizuri katika mahadhimisho ya miaka 55 ya uhuru.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mabati kwa mkuu wa shule ya sekondari Jitegemee kama sehemu ya ahadi yake katika kampeni ya Dar es Salaam mpya.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/=leo jijini Dar es Salaam.
Pia ameweza kuimarisha kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kutoa Zawadi ya Tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi na kutoa zawadi ya gari kwa ajilli ya kuimarisha huduma katika Zahanati ya kikosi cha kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam Ukonga.
0 comments:
Post a Comment