MKUU wa Mkoa Asema kukamilika kwa meli 3 na uwanja wa Ndege wa Songwe kutachochea kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Mbeya na MIKOA YA nyanda za juu kusini
- viongozi wa dini wamepongeza jitihada za uundwaji wa meli mbili za mizigo na moja YA mizigo
- meli za mizigo zimekamilika kwa asilimia 90

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwa mara nyingine amewaalika na kuwashirikisha viongozi wa dini katika ziara yake YA kukagua miradi YA maendeleo na leo wamtembelea Bandari YA Itungi kuona uundaji wa meli Tatu kwa ajili YA mizigo na abiria

Amesema kati YA meli hizo meli mbili ni za mizigo na zina uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja na zitafanya Safari bandari za mikoa YA Njombe , Ruvuma na nchi YA Malawi hivyo zitasaidia kusafirisha bidhaa na malighafi YA viwanda vya Mkoa wa Mbeya na MIKOA YA nyanda za juu kusini .
Meli YA abiria itaitwa Mv Mbeya na itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani za mizigo 200

Aidha meli za mizigo zit sites Mv Njombe na Mv Ruvuma zitaanza Safari mapema mwezi Februali na ile YA abiria itakamilika machi mwakani
Amewaomba wananchi kuchangamka fursa za biashara mara meli hizo zitakapoanza kutumika. 

Amewaeleza viongozi wa dini kuwa Mkoa wa Mbeya utakuwa na fursa Nyingi kupitia usafiri wa meli na pia uwanja wa Ndege wa Songwe hivyo wananchi wajiandae kutumia miundombinu hiyo kama fursa

Kwa upande wa viongozi wa dini wamepongeza jitihada za serikali na hatua za Mkuu wa Mkoa kuwashirikisha ktk ziara zake wamehaidi kuwahamasisha waumini wao kutambua jitihada hizo za serikali na kutumia miundombinu hiyo kama fursa katika kujipatia kipato

0 comments:
Post a Comment