Tuesday, December 27, 2016

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Antony Mavunde ameongoza maelfu ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na wadau wa tasnia ya habari nchini katika maziko ya aliyekuwa mpiga picha wa kampuni ya The Guardian marehemu Mpoki Bukuku.

Marehemu Bukuku alifariki dunia Desemba 23 mwaka huu kwa kugongwa na gari katika eneo la Mwenge jijini Dar es salaam. 
Maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya nyumbani kwao yaliyoko Msalato mjini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.
Marehemu Mpoki Bukuku aliagwa kwa mara ya kwanza jana jijini Dar es salaam kabla ya mwili wake kusafirishwa hadi mjini Dodoma kwa ajili ya maziko.
Akizungumza wakati akitoa salamu zake za rambirambi Mavunde ambaye pia ni ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu amesema enzi za uhai wa marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Dodoma na taifa kwa ujumla kupitia tasnia ya habari.
Marehemu Mpoki Bukuku amefariki akiwa na umri wa miaka 44 akiwa ameacha mke na watoto watano.

0 comments:

Post a Comment