Tuesday, December 20, 2016

Muigizaji wa kike wa filamu za kitanzania Shamsa Ford, amewataka wanawake kujiamni na kujikubali jinsi walivyo, na kuachana na kutumia vitu feki kuonesha urembo wao.

Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa amepost video ikimuonesha binti akicheza muziki club na kuangukwa na magodoro aliyoyaweka kwenye makalio, kisha kuandika ujumbe mzito akiwaasa wanawake kujiamini na kukubali uumbaji wa Mungu.
“Wanawake wenzangu hebu tujiamini jamani na tuuamini uumbaji wa Mungu, Mungu ana sababu ya kukuumba hivyo ulivyo, kama wewe ni mweusi baki na weusi wako, kama huna shape kama mimi baki hivyo hivyo, maana wengine ndo wanachoma masindano ya kuongeza makalio au hips, mwisho wa siku unapata cancer”, aliandika Shamsa.
Shamsa aliendelea kwa kuandika kuwa yeye binafsi anajikubali na ana amini Mungu ana kila sababu ya kumuumba hivyo alivyo, hivyo hata ukimsema vibaya kwa jinsi alivyo hajali.
“Mimi najiamini kupitiliza kama utaona kasoro zangu huwa sijali kabisaa, kwa sababu huwa naamini Mungu ana sababu ya kuniumba hivi nilivyo”, aliandika Shamsa.

0 comments:

Post a Comment