Hujaifaidi Misri kama hujatembelea Mapiramidi ya kihistoria yaliyopo nchini humo. Ndicho alichokifanya Vanessa Mdee baada ya kuzulu katika nchi hiyo.
Vee Money ameshare picha tatu akiwa katika eneo la Mapiramidi hayo na kuelezea namna alivyojisikia kuyaona kwa mara ya kwanza.
“I went on a one man tour of the Pyramids of Egypt today. Ticked that right off my bucket list. This picture describes EXACTLY how I feel. REJUVENATED! #CashMadame #Afrika #Egypt #Pyramids #SheKing,” ameandika Vanessa kwenye picha aliyoiweka Instagram.
Kuna takriban Mapiramidi 118 au 138 nchini Misri, kwa mujibu wa Wikipedia na mengi yalijengwa kutumika kama makaburi kwaajili ya Mafarao na wake zao enzi za kale.
Mapiramidi ya kwanza kabisa yanapatikana kwenye mji wa Saqqara, kaskazini magharibi mwa Memphis. Miongoni mwao ni Piramidi la Djoser lililojengwa kati ya mwaka 2630 BC hadi 2611 BC.
Lakini Mapiramidi maarufu zaidi ya Misri yanapatikana huko Giza, katika vitongoji vya Cairo. Piramidi la Khufu ndilo kubwa zaidi kuliko yote. Ni ajabu pekee la enzi za mababu, lililobaki kati maajabu 7 ya dunia.
0 comments:
Post a Comment