Baada
ya Diamond na Darassa kuchukua baadhi ya vionjo katika nyimbo za Saida
Karoli sasa ni zamu ya Belle 9 ambaye na yeye ametumia baadhi ya vionjo
vya moja ya nyimbo zake kutengenezea wimbo wake 'GIVE IT TO ME'.
Alipozungumza
na eNewz weekend hii wakati akizindua video ya wimbo huo alisema kuwa
wimbo tayari alikuwa ameshaufanya toka kitambo kwa kutumia vionjo hivyo
katika wimbo wa Saida Karoli na sio kwamba amekopi au amefanya kwa
sababu watu wengine wamefanya.
“Mimi
huo wimbo nilikuwa nimeufanya toka muda mrefu na siyo kwamba nimeona
watu wametoa ndiyo nimetoa na wazo hilo nilikuwa nalo toka kitambo sana
pia kuhusu G Nako kuimba sehemu ndogo ni kwa sababu tulikuwa tumegawana
mashairi na siyo kama nimembania” Amesema Belle 9
0 comments:
Post a Comment