Sunday, December 25, 2016

Msanii Chege Chigunda amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zinazofanya achelewe kuachia album yake kuwa ni pamoja na kuzichakachua kazi zake mwenyewe na kuona zinakuwa na kiwango cha juu.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo Chege alisema tayari mpaka sasa album yake imekamilika ila anazidi kuziboresha kazi zake katika album hiyo ili ziwe bora zaidi kwani hataki kutoa album ambayo itakuwa na ngoma ambazo akizisikia mwenyewe ajifiche chini ya meza.
"Unajua kutoa album siyo kutoa 'Single' Radio hivyo nimechelewa kutoa album yangu kwa sababu bado naboresha kazi zilizopo kwenye album hiyo, kwani sitaki nitoe ngoma ambazo mimi mwenyewe nikizisikia nijifiche chini ya meza, hapana najipanga zaidi niweke ngoma kali zote na uongozi utakamilisha mambo mengine na album itawafikia wananchi" alisema  Chege 

0 comments:

Post a Comment